China na Urusi zimendelea kushutumiwa vikali kwa kutumia kura ya turufu kupinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la kumaliza ghasia nchini Syria, ambako mauaji dhidi ya waandamanaji yanaripotiwa kuendelea.
Kansela Angela Merkel anaendelea na ziara yake nchini China ambako anatarajiwa kukutana na Rais Hu Jintao baada ya kukutana na Waziri Mkuu Wen Jiabao aliyemwambia kuwa China ina imani na sarafu Euro.
Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanapiga kura zao leo mjini Addis Ababa kumchagua Mwenyekiti wa Kamisheni ya umoja huo, wadhifa muhimu katika uendeshaji wa masuala ya bara la Afrika.
Wanaharakati wa haki za kibinaadamu wameitisha maandamano nchini Misri kushinikiza utawala wa kijeshi liondoke madarakani, na pia kulaani ghasia za kandanda katika mji wa Port Said.
Viongozi wakuu wa Umoja wa Afrika wamechagua Rais wa Benin, Thomas Boni Yayi, kuwa mwenyekiti mpya wa Umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja kuchukua nafasi kutoka kwa rais wa Guinea ya Ikweta, Teodoro Obiang Nguema.
Maafisa wa ngazi ya juu wa usalama na ulinzi duniani wanakusanyika mjini Munich kuhudhuria mkutano utakaodumu kwa muda wa siku tano mwishoni mwa juma hili huku masuala ya Mashariki ya Kati na Iran yakitawala.
Kansela Angela Merkel anafanya ziara ya siku tatu nchini China. Mada kuu katika mazungumzo pamoja na viongozi wa China ni pamoja na mgogoro wa Syria, mgogoro wa kanda ya Euro, Iran na ushirikiano wa kiuchumi.
Jumuia ya nchi za kiarabu imelisihi baraza la usalama lipitishe hatua dhidi ya utawala wa Syria,lakini Damascus na mshirika wake Urusi hawaonyeshi kuregeza kamba.
Kuanzia Jumatatu ya Februari 6, 2012, Deutsche Welle inajitokeza kwa sura mpya katika mtandao kwa kutumia anuani mpya ya www.dw.de; ruwaza mpya na matangazo ya TV yaliyofanyiwa marekebisho makubwa.
Kutakuwa na mechi mbili nchini Guinea ya Ikweta ambapo Zambia na Sudan wataumiza nyasi katika mji wa Bata na kisha mchuano baina ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Cote d'Ivoire mjini Malabo katika robo fainali.
Magazeti ya Ujerumani yanazungumzia mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, majadiliano kuhusu Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mkutano wa ujumuisho nchini Ujerumani.
DW sasa inakujia katika sura mpya, nembo mpya na sauti mpya.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.de.
Sikiliza makala ya Afrika Wiki Hii na Mohammed Abdulrahman.
Fuatilia michezo ya kuigiza kwa vijana kupitia DW ujuwe maisha ya kila siku barani Afrika.
Tembelea DW katika Twitter
Tembelea DW katika Facebook
Pata huduma zetu kupitia za SMS, RSS, Kijarida na huduma nyengine za mtandaoni kutoka DW.