1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Idadi ya watu wanaofunga ndoa Ujerumani yapungua

2 Mei 2024

Idadi ya watoto wanaozaliwa na ile ya watu wanaofunga ndoa nchini Ujerumani, imepungua mnamo mwaka 2023 hadi kufikia kiwango cha chini kabisa katika kipindi cha miaka kadhaa sasa.

https://p.dw.com/p/4fQFh
Maharusi wakivishana pete baada a kula kiapo cha ndoa
Maharusi wakivishana pete baada a kula kiapo cha ndoaPicha: Royal Hashemite Court/REUTERS

Taarifa hii imetolea na Ofisi ya Takwimu ya Shirikisho ambayo imesema watoto 693,000 walizaliwa nchini Ujerumani mwaka jana, ikiwa ni kiwango cha chini zaidi tangu mwaka 2013.

Idadi hiyo ilipungua kwa asilimia 6.2 ikilinganishwa na mwaka uliopita, ambapo watoto 738,819 walizaliwa.

Soma pia:Rais wa Ujerumani kuanza ziara nchini Uturuki

Mwaka jana, idadi ya watu wanaofunga ndoa imepungua pia kwa asilimia 7.6 ambapo watu 361,000 waliorodheshwa kama wanandoa.

Vikwazo vilivyowekwa wakati wa kupambana na janga la UVIKO-19 vinatajwa kuchangia hali hii.