1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Watu 13 wajeruhiwa Odessa kufuatia shambulio la Urusi

2 Mei 2024

Shambulio la kombora la Urusi limepelekea watu 14 kujeruhiwa katika mji wa Odessa Kusini Magharibi mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4fQGk
Ukraine, Odessa | wafanyakazi wa zima moto.
Kikosi cha kuzima moto Ukraine kikizima moto baada ya shambulio la UrusiPicha: State Emergency Service of Ukraine/Anadolu/picture alliance

Hayo yameelezwa na Meya wa jiji hilo Gennadiy Trukhanov ambaye ameongeza kuwa vikosi vya uokoaji vilikuwa vikikabiliana na moto mkubwa bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Mji wa Odesa, wenye bandari kwenye Bahari Nyeusi ni muhimu kwa mauzo ya nje ya Ukraine, na umekuwa ukilengwa mara kwa mara na mashambulio mabaya ya Urusi.

Jana, maafisa katika mji huo walisema watu watatu waliuawa katika shambulio la kombora la Urusi.

Soma pia:Makombora ya Urusi yauwa watu watano Ukraine

Ukraine imesema pia kuwa imeharibu kiwanda cha kusafisha mafuta cha Urusi huko Ryazan, takriban kilometa 200 kusini-mashariki mwa mji wa Moscow.